1 Chronicles 6:31-33

Waimbaji Wa Hekalu

31 aHawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya Bwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. 32Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la Bwana huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

33 bWafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:

Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa:
Hemani, mpiga kinanda,
alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,
Copyright information for SwhNEN